Mbunge wa Jubilee apanga kuuza helikopta ya Gavana wa ODM na nyumba ya KSh140 million

- Mbunge wa Kilifi North Gideon Mungaro amemsuta Gavana wa Kilifi Amason Kingi - Mbunge huyo mlimi sana anasema ataiuza nyumba ya Kingi ya thamani ya KSh 140 milioni na helikopta yake akichaguliwa kuwa Gavana wa Kaunti ya Kilifi

- Mbunge wa Kilifi North Gideon Mung’aro amemsuta Gavana wa Kilifi Amason Kingi

- Mbunge huyo mlimi sana anasema ataiuza nyumba ya Kingi ya thamani ya KSh 140 milioni na helikopta yake akichaguliwa kuwa Gavana wa Kaunti ya Kilifi

- Mung’aro na Kingi kwa muda mrefu wamekuwa mahasimu wakubwa wa kisiasa

Mbunge maarufu wa Kilifi North Gideon Mung’aro ameziimarisha kampeni zake na kwa sasa, amemtikisa mpinzani wake, kwa kuzilenga kampeni zake dhidi yake.

Habari nyingine: Rais Uhuru atapeliwa KSh 800,000, pata uhondo

TUKO.co.ke tulivyoripoti mapema, Mbunge huyo alihama ODM na kuingia Jubilee na kutangaza azma yake ya kutaka kuwa Gavana wa Kaunti ya Kilifi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.

Mungaro, kwenye kampeni yake majuzi, alisisitiza kuwa yeye ndiye anayeweza kumwangusha Gavana wa sasa Kilifi Amason Kingi kwa kuwa ana matakwa yatakayowafaa wakazi wa Kilifi.

Habari nyingine: Wakuu wa muungano wa madaktari wahukumiwa kifungo gerezani huku mgomo ukichacha

Akiwa Chakama, Kaunti ndogo ya Malindi Ijumaa, Aprili 7 2017, Mung’aro alisema hataishi maisha ya kitajiri na ufahari na kuacha wenyeji katika ufukara, atakapochaguliwa kuwa Gavana Agosti 8.

Aidha Mbunge huyo mlimi sana alisema ataiuza nyumba ya Kingi ya thamani ya KSh 140 milioni na helikopta yake akichaguliwa kuwa Gavana wa Kaunti ya Kilifi na pesa zitakazopatikana atazitumia kuwafaa watu wake.

Habari Nyingine: Jubilee yapuuzilia mbali kuundwa kwa muungano wa NASA

Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!

“Nitakuwa naishi nyumbani kwangnu Dabaso. Hamna haja ya kuwa na kifaa kama kile ambacho kina gharama kubwa kwa walipa kodi,” alisema Mung'aro.

Subscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos!

Kulingana naye, nyumba ya KSh 140 milioni na helikopta ni hasara kubwa ambayo ni pesa za umma.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaIN5gJdmpJutnpyybsPAZqGumpmhsqZ5wKmYp5%2BRYri2wdmaZKGdnJ64sLzTmmSymV2crretzZpksJldpLGuec2aZKexpaKvonnYmmSkq5hmgW%2B006aj

 Share!