Mambo ya kuudhi ambayo Wakenya wanapaswa kuyaacha mwaka wa 2017

-Kenya imepitia mambo mengi mwaka huu wa 2017 yakiwemo ya siasa ,burudani na kadhalika - TUKO .co.ke iliweza kuangazia mambo kadhaa ambayo wakenya hawapaswi kuvuka nayo hadi mwaka wa 2018 Haya ndio mambo 11 ambayo kila Mkenya anafaa kuyaepuka ifikapo mwaka wa 2018

-Kenya imepitia mambo mengi mwaka huu wa 2017 yakiwemo ya siasa ,burudani na kadhalika

- TUKO .co.ke iliweza kuangazia mambo kadhaa ambayo wakenya hawapaswi kuvuka nayo hadi mwaka wa 2018

Haya ndio mambo 11 ambayo kila Mkenya anafaa kuyaepuka ifikapo mwaka wa 2018

1.Odi Dance

Aina hii ya kusakata densi imevuma katika kila sehemu ya nchi na imependwa sana na vijana wengi

2. Sarakasi za ‘ Boy child na Girl child'

Kama ilivyo kawaida kila mtu ameshuhusi sarakasi hizo na zinapaswa kusalia mwaka wa 2017.

3.Siasa za Jubilee na NASA

Ikizingatiwa kuwa rais ashapatikana, wanasiasa wanapaswa kukuza maendeleo ya nchi badala ya siasa ambazo kwa sasa hazina umuhimu.

4 Misemo zinazoudhi kama’ Manenos na Issa’

Misemo hii hutumika sana na ma 'Slay queen' na vijana wanaopenda kutumia sana mitandao ya kijamii

5. Mienendo ya slay queens kupigwa picha kila mara

Wasichana ambao hujiona warembo kila mara hushinda wakipiga picha nyingi kila mara na kuzijaza mitandaoni.

Mtindo huu unapaswa kurekebishwa kwani unaudhi sana.

6. Kuweka jumbe za uwongo mitandaoni

Watu wengi wana mazoea ya kudanya kuhusu maisha yao au kudanya kuwa wako mahali Fulani hasa katika sehemu za kifahari ila si hivyo

7.Mazoea ya kuiga mtu maarufu anapofanya jambo lisilo la kawaida

Wakenya wana mtindo wa kuiga jambo lolote linapotokea ambalo sio la kawaida,kwa mfano jinsi wavinya ndeti alivyoteleza ulimi na kusema, ‘ Yaliopita si ndwele’

8 Watalaam wa kukashifu

Mtu yeyote hasa mwanasiasa ,mwanamuziki wanapofanya jambo lolote liwe baya au nzuri ,hukashifiwa katika kila hali.

9. Wakenya kuweka hadharani maisha yao mitandaoni

Sio kila mtu hufurahishwa unapoanika maisha yako mitandaoni,ni wachache sana watatakajua jinsi unavyoishi.

Mtindo huu sio wa maendeleo na ni vyema uachwe mwaka huu.

10. Kasumba ya kuudhi

Tabia ya Wakenya kuingilia jamii zingine kwa kutokana na mazoea yao,kama vile waluhya husemekana wanapenda chakula na Wakikuyu wanapenda pesa

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia356f5JmpJqlkqR6uq2MpKyunJieeqK5wZqwqGWnlrimutiaZLCZnpa9or%2FWmmSkramWrqS0wGaksJmblnq4rYxrZ2pvXp3Brrg%3D

 Share!