Mkahawa wapuzilia mbali maandamano dhidi yake kwa kumtaka mwanamke kunyonyesha mtoto ndani ya choo

-Usimamizi wa mkahawa wa Olive ulishutumu maandamano yaliyokuwa yamepangwa -Mkahawa huo pia ulipuzilia mbali madai ya mwanamke huyo kwa kusema ulimwomba kufunika mtoto wakati wa kunyonyesha -Mkahawa huo ulisema haujapokea malalamishi rasmi kutoka kwa mwathiriwa baada ya mwanamke huyo kulalamika katika mtandao wa kijamii kwamba alilazimishwa kumnyonyesha mwanawe chooni

-Usimamizi wa mkahawa wa Olive ulishutumu maandamano yaliyokuwa yamepangwa

-Mkahawa huo pia ulipuzilia mbali madai ya mwanamke huyo kwa kusema ulimwomba kufunika mtoto wakati wa kunyonyesha

-Mkahawa huo ulisema haujapokea malalamishi rasmi kutoka kwa mwathiriwa baada ya mwanamke huyo kulalamika katika mtandao wa kijamii kwamba alilazimishwa kumnyonyesha mwanawe chooni

Mkahawa mmoja ambao hivi majuzi uliibua mjadala mkubwa kwa kumtaka mwanamke kunyonyesha ndani ya choo umetoa taarifa.

Habari Nyingine: Ng’ombe ajifungua ndama mwenye miguu 2 Bungoma

Kama ilivyoripotiwa awali, Betty Kim, alieleza alivyolazimishwa kumnyonyesha mwanawe ndani ya choo na wahudumu wa Olive Restaurant, katika barabara ya Accra, Nairobi.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Kisa hicho kilitokea Jumatatu, Mei 7, alieleza Betty. Hoteli hiyo hata hivyo katika taarifa Ijumaa Mei 11, ulikana madai hayo yaliyowekwa katika kundi la Facebook Buyer Beware (Kenya) na kueleza kuwa kuwa Betty aliombwa kumfunika mtoto wake.

Habari Nyingine: Aina 5 za kina dada na tabia zao za kushangaza kanisani

Usimamizi wa hoteli hiyo ulieleza kuwa bado haujapokea malalamishi rasmi kutoka kwa mwathiriwa, na kusema ulibaini kisa hicho kupitia mtandao wa kijamii.

Mkahawa huo ulipuzilia mbali maandamano yaliyopangwa na kundi hilo la Facebook kwa kusema hoteli hiyo haikupewa nafasi ya kujitetea au kufanya uchunguzi.

Habari Nyingine: Picha za bintiye Gideon Moi ni thibitisho kwamba ni mrembo kupindukia

Ilisema kuwa kundi hilo linalenga kuuharibia jina na kusema utachukua hatua. Wakenya wengi walishutumu kitendo hicho na kuukosoa sana mkahawa huo.

Baadhi yao waliwataka marafiki na jamaa kususia chakula na huduma hotelini humo.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Subscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIB2hJNmpKSZmJbEonnWmqeuspmhtqJ5zJuYpaFdoq6iusOapJqmn2KxqbXDomSymZuaeqzDwGairqWklriiecywmKeZnaCybrfUp7CopqmawKmtjKarqKyfYrulrc2iZLKZXZi1sLuNoaumpA%3D%3D

 Share!