Viongozi wa ODM waapa kumkabili waziri Rashid Echesa baada ya kumshambulia Raila

-Waziri wa michezo Rashid Echesa huenda akaandamwa na masaibu baada ya kumshambulia Raila -Viongozi wa ODM wamekashifu matamshi ya Echesa dhidi ya kinara wa chama chao -Hivi majuzi, Echesa alidai kuwa Raila alikuwa akitatiza kazi yake kama waziri

-Waziri wa michezo Rashid Echesa huenda akaandamwa na masaibu baada ya kumshambulia Raila

-Viongozi wa ODM wamekashifu matamshi ya Echesa dhidi ya kinara wa chama chao

-Hivi majuzi, Echesa alidai kuwa Raila alikuwa akitatiza kazi yake kama waziri

Huenda matamshi makali ya hivi punde ya waziri wa michezo Rashid Echesa dhidi ya Raila Odinga yakamwathiri huku dalili za mabadiliko kwenye baraza la mawaziri yakiashiriwa.

Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM Jumapili, Agosti 5 walitoa onyo kali kwa Echesa kwa kukosa kumheshimu kinara wa chama chao.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Mwanamke akutwa akiiba TV mtaani, arekodiwa kwenye video akipata kichapo cha mbwa koko

Wakiongozwa na katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna, viongozi hao walisema kuwa Echesa hakuiwakilisha jamii ya Waluhya kikamilifu na matamshi yake dhidi ya Raila yatamsababishia adhabu kali.

Mbunge maalum Godfrey Osotsi alimpa Echesa saa 48 kumuomba Raila msamaha au sivyo awasilishe hoja bungeni ya kumwondoa ofisini.

“Ikiwa hutaomba msamaha chini ya saa 48, tunahakikisha umeondolewa ofisini kwa hoja bungeni,” Osotsi alisema.

Habari Nyingine: Mkenya Akuku Danger na wanaume 10 walioandikisha rekodi ya kuwa na watoto wengi zaidi duniani

Kama TUKO.co.ke ilivyoripoti hapo awali, Echesa aliyezungumza kwenye hafla ya mazishi kijijini Musanda, Mumias Mashariki katika kaunti ya Kakamega alidai kuwa Raila aliwachochea viongozi wa jamii ya Waluhya na hata Rais Uhuru Kenyatta dhidi yake kwa msingi kuwa alitembea sehemu tofauti na kutangaza kuwa yeye ni mwandani wa naibu wa rais William Ruto.

Alisema kuwa matamshi yake yangemwathiri kwa njia tofauti, ikiwemo kupoteza kiti chake.

“Ninataka kuwa wazi nawe Raila. Ninakuheshimu sana lakini naomba ukome kutumia jina langu ovyo. Mimi sio mtu wa hadhi yako. Rais hakukosea aliponiteuwa kuwa waziri ingawa alikuwa kuwa mimi sio profesa aliyefuzu,” Echesa alisema.

Huenda matamshi ya Echesa yalitokana na habari kuwa Raila Jumanne, Julai 31 alifanya mkutano eneo la Magharibi ambapo hakuhusishwa.

Habari Nyingine: Daktari wa kike kutoka Cuba anaswa kwenye video akisakata ngoma kiajabu, Tana River

Hata hivyo, Sifuna alidai kuwa Raila ndiye aliyemsaidia Echesa kupata kazi yake na kuwa alistahili kumshukuru waziri huyo mkuu.

“Mtu wa kwanza kukiri talanta ya Echesa alikuwa Raila. Ikiwa hangekuwa kiongozi wa vijana wa ODM, basi watu hawangelijua jina lake,” Sifuna alisema.

Habari Nyingine: Betty Kyalo awaacha 'team mafisi' kwa mate midomoni kwa kunengua kiuno kwa madaha

Huenda uhusiano mbaya kati ya Echesa na Raila ambaye ni mshirika wa hivi punde wa Rais Uhuru Kenyatta ukamfanya apoteze wadhifa wake baada ya kupoteza umaarufu kwenye chama cha ODM.

Kumekuwa na fununu kuwa huenda baraza la mawaziri likafanyiwa mabadiliko baada ya sakata kadhaa za ufisadi kufichuliwa hivi majuzi.

Mawaziri Najib Balala (utalii), Willy Bett (kilimo), Henry Rotich (fedha) na Sicily Kariuki (afya) wameangaziwa kutokana na sakata hizo za ufisadi.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Raila Odinga ni mradi chini ya Rais Uhuru Kenyatta | TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibX56fJFmraKnnpy8u7WMsJhmp5SieritwKmYZqOloriirsiloGavka%2B2s7WMq5isoJmZeqavx56qmmWSlq6lrYyymGajpaLAqa3Mm6yloZFiv6K1y5ploaydoQ%3D%3D

 Share!