Mbunge wa Suba Millie Odhiambo Jumatano, Septemba 4, aliwasha moto kwenye mtandao baada ya kumwanika jamaa ambaye alikuwa amemmezea mate kiwango cha kuingia kwenye DM yake na kujaribu kupapasa moyo wake.
Millie, ambaye anajulikana kwa kuanika wazi kiu yake ya penzi tamu, aliwaacha wengi wamechangamka kwa kusimulia vile ndume huyo alivyoangusha mistari.
Habari Nyingine: Sonko asifia EACC kwa kumhoji ipasavyo, asema yuko tayari kujiuzulu akipatikana na kosa
“Mimi hukutamani sana. Mimi hukufuatilia sana haswa kazi yako kwenye kikosi cha akina mama cha Embrace. Natoka Marekani lakini nitakuwa kwenye ziara nchini Kneya na ninaweza kukuunganisha na watu wanaoweza kufadhili Embrace, na pia natamani nikutane nawe," jamaa huyo alimwambia Millie ndani ya DM yake.Millie alisema hakuonyesha mvuto wowote kwa ndume huyo lakini aliendelea kumnyemelea huku akimpa picha moja akiwa kifua wazi labda katika juhudi za kusisimua hisia zake Millie.
Habari Nyingine: Demu akaripiwa na wazee kwa kuchukua mkopo kujilipia mahari
Mbunge huyo aliwafahamisha ndume ambao huenda wanamsaka kuwa ametupa makali ya penzi kutokana na umri wake na kwa hivyo kuna haja ya wao kuwinda kwingine.
"Wanaume tafadhali, katika umri wangu sasa nafikiria ni kina nani wanawachumbia wapwa wangu. Kama ningalikuwa mwanaume, ningesema kuwa upanga sasa umepata kutu," alisema Millie.READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 073248269
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZoF2gpFmpKKknJ6ybrvDoaCapZKkeqK51pqloqORYreiucCaZJqkma6yrMHWmmSao5miuqbGxJpkppmkmnupwMyl