Magazeti ya Alhamisi, Aprili 23: DP Ruto apoteza shamba lake la Ruai

Magazeti ya Jumanne, Aprili 23, yanaongoza na msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta ya kutupilia mbali wazo la kufungwa kwa shughuli zote nchini huku idadi ya visa vya corona ikifika 300. Kurejeshwa kwa hekari 1,600 ya ardhi mtaa wa Ruai ambayo ilikisiwa kunyakuliwa na watu wenye ushawishi mkubwa serikalini na Gavana Sonko kujutia kupeana uongozi wa

Magazeti ya Jumanne, Aprili 23, yanaongoza na msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta ya kutupilia mbali wazo la kufungwa kwa shughuli zote nchini huku idadi ya visa vya corona ikifika 300.

Kurejeshwa kwa hekari 1,600 ya ardhi mtaa wa Ruai ambayo ilikisiwa kunyakuliwa na watu wenye ushawishi mkubwa serikalini na Gavana Sonko kujutia kupeana uongozi wa jiji la Nairobi pia ni taarifa kuu katika magazeti haya.

Habari Nyingine: Madaktari na wauguzi wakimbilia usalama wao baada ya mwenzao kudai anaugua COVID-19

Habari Nyingine: Ken Walibora alitofautiana vikali na mchapishaji wake kabla ya kifo chake, DCI yafichua

1. People Daily

Gazeti hili linaripoti kuwa hekari 1,600 ya shamba katika eneo la Kangundo ambalo lilichukuliwa na serikali siku ya Jumatano, Aprili 22, linamhusisha Naibu Rais William Ruto.

Kulingana na idara ya serikali kuhusu Ardhi na Upangaji, kipande hicho cha ardhi ni cha serikali ambacho kilikuwa kinatazamiwa kutumika katika kupanua kampuni ya kutibu maji taka Nairobi.

Ruto, kupitia kampuni ya Renton, alikabithiwa sehemu ya ardhi hiyo katika mtaa wa Ruai mwaka 1995 na aliyekuwa Waziri William ole Ntimama.

Kipande cha pili cha ardhi hiyo kinahusisha kampuni inayomilikiwa na Mbunge wa zamani wa Lugari, Cyrus Jirongo ya Offshore Trading.

2. Taifa Leo

Katika gazeti hili, Wakenya ndio watu wanaohangaika kwani wanakumbana na majanga kila upande.

Wakati mwaka huu ulipoanza, taifa hili lilivamiwa na nzige wa jangwani ambao wameharibu mimea katika maelfu ya mashamba.

Hii ni baada ya mvua kubwa ulionyesha nchini mwishoni mwa mwaka jana na kuwaacha maelfu bila makao na wengine kufariki.

Kaunti ambazo ziliathirika ni Elegeiyo Marakwet, Kisumu na Pokot Magharibi.

Ghafla bin vuu, janga la virusi vya corona lilibisha na kuathiri vibaya uchumi katika njia ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Mvua pia umerejea na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 12 katika kaunti za Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi.

Mamia ya wakazi Kisumu wamepoteza makazi yao baada ya nyumba zao kusombwa na maji.

3. The Star

Hazina ya Taifa imefichua kuwa imetumia KSh 40 bilioni katika vita dhidi ya virusi vya corona tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza nchini mnamo Ijumaa, Machi 13.

Hii ina maana kuwa katika kipindi cha siku 40 taifa hili limekuwa likitumia KSh 1 bilioni kila siku katika kukabiliana na janga hilo.

Zaidi ya KSh 33.4 bilioni ziliwekwa katika zoezi hilo huku KSh 6.9 bilioni zikiwekezwa katika miradi tofauti ya kupambana na ugonjwa huo wa kupumua.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Taifa, Justine Mutura amebainisha kuwa hakuna mbunge yeyote alipatwa na virusi hivyo baada ya kupimwa pamoja na wafanyakazi wengine wa bunge.

4. The Standard

Gazeti la The Standard linaripoti kuwa Naibu Rais mnamo Jumanne, alifanya mkutano na Gavana wa Nairobi, Mike Sonko katika makazi yake ya Karen ambapo walijadiliana kuhusu uongozi wa jiji hilo.

Sonko alichukuliwa na Mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi kutoka kwa makazi yake ya Upper Hill na kuenda kukutana na Ruto katika mkutano ambao uliendelea hadi usiku wa manane.

Baada ya mkutano huo, Sonko mnamo Jumatano alisema kuwa atafanya majadiliano ambapo atarejeshewa uongozi wa jiji baada ya kushuhudiwa akimkabithi Jenerali Mohamed Badi huduma muhimu za kaunti.

Gavana huyo alisema yuko tayari kuuawa ama hata kufungwa jela wakati wa mchakato huo huku akidai kwamba alishinikizwa kutia saini uamuzi huo.

5. Daily Nation

Walioajiriwa nchini Kenya wanatazamiwa kupata mishahara zaidi mwishoni mwa mwezi huu kufuatia mabadiliko mapya ya kutozwa ushuru wa PAYE yalioamrishwa na Rais Uhuru.

Uhuru alisema hatua hiyo inapania kuweka pesa katika mifuko za Wakenya ili kuwalinda kutokana na kudorora kwa uchumi iliyosababishwa na janga la virusi vya corona.

Wale ambao walikuwa wakilipwa mishahara ya KSh 24,000 kila mwezi kwa sasa watapata pesa zingine KSh 1,583 zaidi.

Waajiriwa wanaopata KSh 30,000 yamkini wataweka KSh 2,000, wale wa KSh 40,000 watabaki na KSh 2,400 zaidi huku wale wanaolipwa KSh 50,000 kupata KSh 3,400 zaidi.

Endapo unalipwa KSh 75,000, unatazamia kupata KSh 4,500 zaidi katika akaunti yako, KSh 100,000 (KSh 5,800) huku wale wanaoingiza kibindoni KSh 200,000 hadi KSh 300, 000 watapata KSh 10,000 na KSh 15,000 zaidi.

Hata hivyo, rais bado hajatia saini mabadiliko hayo lakini endapo bado yuko hai basi mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaoByhJJmpJqfka%2BytbWMsphmmZydrq610qJkmqiinrmqeZFsZJ2oXafCtbuMmqeorJWvrm6%2Fx5qkm5ldoa6ssYylmGaqpZa2b7TTpqM%3D

 Share!