Magazeti ya Jumatano, Disemba 30, yanaripotia kuwa mwaka 2021 utakuwa mgumu kwa Naibu Rais William Ruto kwani atafanya maamuzi ambayo yatajenga ama kusambaratisha azma yake ya kuwania urais.
Fauka ya hayo, magazeti haya pia yameripotia pakubwa kuhusu uchaguzi mdogo wa Februari 18, 2021, wa kiti cha ugavana Nairobi na kujiondoa kwa ODM kwenye kivumbi hicho.
Habari Nyingine: Miguna Miguna aanika manifesto yake 7 atakayotimiza akichaguliwa gavana
Habari Nyingine: Arsenal wasajili ushindi wa pili kwa mpigo na kumuondolea Mikel Arteta presha
1. Daily Nation
Kulingana na gazeti la Daily Nation, Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimeamua kujiondoa kwenye kivumbi cha kiti cha ugavana Nairobi ili kumuunga mkono mgombea wa Chama cha Jubilee.
Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama hicho John Mbadi alisema chama hicho kinafanya mazungumzo na chama tawala ambacho kinapania kuhifadhi kiti hicho kilichosalia wazi kufuatia kung'atuliwa kwa Mike Sonko mnamo Alhamisi, Disemba 17.
Hii inamaanisha kuwa ODM kitampigia debe mbunge wa zamani wa Dagoretti Kusini Dennis Waweru ama mwanabiashara Agnes Kagure ambao majina yao yaliwasilishwa kwa IEBC kama waniaji katika kura ya mchujo.
Haya yanajiri huku ikiibuka kuwa ODM kilishindwa kuwasilisha majina ya wagombeaji wake kwa IEBC kufikia Jumatatu, Disemba 28, ambapo ilikuwa siku ya mwisho.
2. The Standard
Gazeti hili linaripotia jinsi Naibu Rais William Ruto anakabiliwa na kibarua kigumu huku uchaguzi mkuu wa 2022 ukinusia.
Ruto kwa sasa yuko njia panda baada ya wandani wake kubadilisha jina la chama kilichokuwa kinahusiana naye awali cha Party for Reforms Development kuwa United Democratic Alliance (UDA) chini ya kauli mbiu Kazi ni Kazi.
Ruto amebanwa katika uamuzi wa kuhama Chama cha Jubilee, kukabiliana na watesi wake na kupigia debe azma yake ya urais 2022 ama kusalia Jubilee na kustahimili baridi.
Kulingana na wachanganuzi wa siasa, 2021 utakuwa mwaka mgumu kwa Ruto ambapo anatazamiwa kufanya uamuzi ambao utamsaidia kuwa rais.
3. Taifa Leo
Kulingana na Taifa Leo, kamishna wa kaunti ya Mombasa amewaambia wakazi kuwa sheria ya kafyu itaendelea kutekelezwa kwenye mkesha wa Mwaka Mpya.
Gilbert Kitiyo alisema mwaka huu wakazi wa Pwani hawatatangamana pamoja kukaribisha mwaka mpya kama ilivyokuwa desturi.
Kitiyo aliwashauri wakazi kukaribisha mwaka mpya kupitia runinga ili kujiepusha na kukiuka sheria.
Baadhi ya Wakenya wamekuwa wakimuomba Rais Uhuru Kenyatta kulegeza baadhi ya masharti ya COVID-19 mnamo Disemba 31, ili kukaribisha mwaka mpya kwa mbwembwe.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjboV0gJNmpJqfka%2BytbWMsphmoqWirrWtzahknaGjmrqjrYxsZ2anlKJ6pLTAo6CoppSkrm631p6lsp1dqrCprcausaJlnZm8qLuMp5iiqp%2BXtm%2B006aj