- Wagonjwa wengine 26 wamepona ugonjwa huo na kuongezea idadi ya waliopata nafuu kuwa 82,350
- Japo si kwa kasi, idadi ya vifo imepanda hadi 1,731, kufuatia kifo cha wagonjwa wengine watatu kati ya Jumamosi na Jumapili
- Taifa bado linasubiri kwa hamu na ghamu chanjo ambapo shehena ya kwanza inatazamiwa kuwasili nchini mwezi ujao kulingana na Waziri Kagwe
Habari Nyingine: Mombasa: Utamu wamzidia jamaa aliyekuwa akishiriki penzi na kufariki dunia
Idadi jumla ya visa vya COVID-19 nchini Kenya imeongezeka hadi 99,162 baada ya watu 80 kuambukizwa, Wizara ya Afya imetangaza.
Akitangaza visa hivyo vipya siku ya Jumapili, Januari 17, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema wagonjwa hao waligunduliwa baada ya sampuli 3,733 kupimwa kati ya Jumamosi na Jumapili.
"Jumla ya vipimo vilivyofanywa kufikia sasa ni 1,125,679. Kutoka kwa visa hivyo, 62 ni Wakenya huku 18 ni raia wa kigeni," alisema Kagwe.
Habari Nyingine: Rais Museveni ajilinganisha umri na Bobi Wine, adai hasidi wake ni mzee
Kagwe pia alithibitisha kuwa wagonjwa wengine 26 wamepona ugonjwa huo na kuongezea idadi ya waliopata nafuu kuwa 82,350.
Japo si kwa kasi, idadi ya vifo imepanda hadi 1,731, kufuatia kifo cha wagonjwa wengine watatu kati ya Jumamosi na Jumapili.
Msambao katika kaunti
Kati ya visa hivyo 80 vilivyorekodiwa Jumapili, 62 ni kutoka Nairobi, Meru (4), Busia na Kwale (visa vitatu kila mmoja) huku Kiambu ikirekodi visa viwili.
Visa vingine ni kutoka Kericho, Kilifi, Makueni, Mombasa, Nyandarua na Uasin Gishu ambazo zilikuwa na kisa kimoja.
Waliolazwa
Kagwe alisema kuna wagonjwa 699 ambao wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku 1,642 wakitibiwa nyumbani.
Wagonjwa 30 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), 14 wamewekewa mashine ya kuwasaidia kupumua na 13 wanaongezewa oksijeni. Watatu wanachunguzwa kwa karibu.
Wagonjwa wengine 13 wamelazwa katika vyumba kawaida 12 kati yao wamo katika wodi za kawaida na kisha mgonjwa mmoja katika chumba cha wagonjwa mahututi zaidi.
Chanjo
Taifa bado linasubiri kwa hamu na ghamu chanjo ambapo shehena ya kwanza inatazamiwa kuwasili nchini mwezi ujao kulingana na Waziri Kagwe.
"Tumezungumza na taasisi kadhaa kama vile GAVI, shirika ambalo linahusika na kusambaza chanjo Kenya kufikia Februari. Hata hivyo kuna uwezekano wa Kenya kupata chanjo hizo mapema."
"Mipango ambayo inafanywa na sekta ya kibinfasi ya serikali inatazamia chanjo hizo zitafika Februari kulingana na GAVI. Pia tumesema hatutatumia aina moja ya chanjo pekee. Washirika wetu wanaohusiana na Moderna, Pfizer, AstraZeneca na chanjo za China kama vile Sinopha wanajadiliana leo kuamua namna chanjo hizo zitafika Kenya," alisema Kagwe.
Maambukizi kimataifa
Kufikia Jumapili, Janauri 17, yamkini watu 95,049,394 wameambukizwa virusi hivyo tangu kulipuka mjini Wuhan, China mwaka 2019.
Zaidi ya watu 2,032,835 wamepoteza maisha yao huku 67,876,639 wakipona.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZX1xgJVmrpqjlaPGonnWnqWgoZ6aenl8jLCYmqWSqriqxtaaZK%2BhoqrAqnnVsphmm5%2BnvK%2BtjKeYZm5pbnqswcuasbCZXp3Brrg%3D