Mumias Mjini: Kisura azua kisanga kuponyoka na kijana wa sponsa

Mzee mmoja kutoka Mumias, kaunti ya Kakamega alijikuta njia panda baada ya kidosho kumshurutisha akubali kuolewa na mwanawe la sivyo aanike siri baina yao. Penyenye zinasema kwamba mzee huyo mpenda michepuko alikuwa na uhusiano wa pembeni na mrembo huyo kwa muda mrefu hadi pale ambapo kisura alikutana na mwana wa buda anayesoma Marekani.

Mzee mmoja kutoka Mumias, kaunti ya Kakamega alijikuta njia panda baada ya kidosho kumshurutisha akubali kuolewa na mwanawe la sivyo aanike siri baina yao.

Penyenye zinasema kwamba mzee huyo mpenda michepuko alikuwa na uhusiano wa pembeni na mrembo huyo kwa muda mrefu hadi pale ambapo kisura alikutana na mwana wa buda anayesoma Marekani.

Habari Nyingine: Uchaguzi wa Kabuchai: Cherargei, Didmus Barasa wakamatwa

Kwa mujibu wa Taifa Leo, jamaa alimrushia mistari kisura akamweleza alitoka familia ya kitajiri na endapo angekubali basi wangiishi maisha ya raha mstarehe.

“Najua fika kwamba jamaa yako kwao wana pesa. Hata hivyo, mambo huhitaji utaratibu. Twende pole pole,” kidosho alimshauri jamaa.

Haukupita muda kabla demu aanze kumpimia penzi mzee naye akaanza kumshuku na kuwalipa makachero wamchungue mienendo yake.

“Mwanao ndiye aliyejishinda kichuna wako ,” makachero walimuarifu mzee.

Habari Nyingine: Matungu: Seneta Cleophas Malala amchapa kofi Gladys Wanga

Ujumbe huo ulimchoma roho mzee ambaye mara moja alifululiza hadi katika nyumba aliyomkodishia kisura.

“Haya ni mambo gani unayonifanyia?Hujui unacheza na nani? Iwapo mwanangu atakuoa, tutaishi vipi?” mzee alinguruma.

“Hiyo ni shida yako. Tuko tayari kuoana hata harusi tushapanga. Utajipanga mzee,” kisura alijibu.

“Kwangu nayo huoelewi! Naapa tena huolewoi kwangu kunyeshe mvu au kuwake jua,” buda alijibu.

“Nitaolewa ukitaka usitake. Ukidhani wewe ndiwe kijogoo, basi nitamweleza mwanao unayempenda kupita kiasi na usiyetaka kumpoteza kwamba tumekuwa na uhusiano wa kimapenzi. Najua hilo usingetaka alijue,” kisura alisema.

Habari Nyingine: London ward: Ghasia zashuhudiwa polisi wakikabili wafuasi wa UDA

“Basi usitamani nitengane na mwanangu. Umeshinda. Hata hivyo fikiria kuhusu penzi letu. Je, nitaendelea kula sahani moja na mwanangu,” buda aliuliza.

“Hapa hutakula tena. Iliyobaki ni ya mwanao pekee,” mrembo anasemekana alimjibu mzee na kumtimua.

Hata hivyo, haikujulikana iwapo kisura aliolewa na mwana wa buda huyo au la.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYF1gZJmpK6lmZbAbrnJoqWiZZuewLa%2BwGaYs62RYriqv8Cnnpplm6q9sLrYqKKaZZ6Weqy1yZqlmmWnlnq0vM6nqppmmKm6rQ%3D%3D

 Share!