- Gavana Charity Ngilu amemshtumu Naibu Rais William Ruto kwa kile alichokitaja kama kumtelekeza Rais Uhuru Kenyatta
- Ngilu alisema Ruto anapaswa kujifikiria tena na atambue anachokitaka la si sivyo ataharibu agenda ambazo anastahili kutekeleza na Rais
- Alimtaka pia Ruto kuonyesha maendeleo ambayo amefanya kwa miaka tisa ambayo amekuwa naibu wa Rais
Gavana wa kaunti ya Kitui Charity Ngilu amemshtumu Naibu Rais William Ruto kwa kumkandamiza Rais Uhuru Kenyatta na kutelekeza ajenda walizokuwa nazo wakiwa uongozi muhula wao wa kwanza.
Habari Nyingine: Kuna Panya Ndani ya Jubilee, Tutawamaliza na Nyumba Kusalia Salama
Ngilu alimkashifu Ruto kwa kuangazia masuala yasio ya maendeleo, kupiga siasa za mapema na kumuachia Rais kufanya kazi pekee.
Gavana huyo sasa amemtaka Ruto kuonyesha maendeleo ambayo amefanya tangu alipochukua hatamu za uongozi miaka tisa iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa za Citizen Digital, Ngilu alisema Ruto anafaa kuweka mpangilio ambao hautasambaratisha ajenda walizoafikiana na Rais kutekeleza.
"" Naibu Rais William Ruto hawezi akasaidia nchi hii, hebu kwanza atuonyesha ni maendeleo gani amefanya kwa miaka 9 ambayo amekuwa uongozini, hebu atuonyesha kiwanda hata kimoja ambacho amezingua.
" Ruto anafaa kujifikiria tena na amsaidie kutimiza ahadi walizowapa wakenya walipokuwa wakitafuta kura. Yeye kujiingiza katika kampeni za mapema za uchaguzi mkuu wa 2022 haisaidii, ila itavunja na kuharibu mipango yote ya serikali," Ngilu alisema.
Ngilu ambaye pia aliwania urais, alifutilia mbali madai kwamba ajenda kuu ya yeye kuzuru Ikulu hivi maajuzi ilikuwa ni kujadili na Rais kuhusu siasa za urithi.
Kulingana na Ngilu, mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi ya viongozi kutoka mkoa wa Mashariki ulikuwa ni wa kumjuza Rais kuhusu maendelea eneo hilo na jinsi atakavyowasaidia kuyatekeleza kwa haraka.
Habari Nyingine: Gavana Waiguru Awafunza Wanafunzi Kusakata Densi ya Wimbo Sukari
Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Rais Uhuru Kenyatta alifanya mkutano na viongozi kadhaa kutoka eneo la Ukambani katika Ikulu ya Nairobi, ajenda kuu ilikuwa ni kujadili kuhusu maendeleo.
Aliyekuwa makamo wa Rais Kalonzo Musyoka alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano.
Kalonzo ni miongoni mwa wanasiasa ambao wametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoJ3hJhmnpqukaOubrrGoqOuZZGiuKK%2Fx6KdrmWUpXqzwdOoZKSvkWK4tsDAp56aZaSWu6itjJuYnZmclnq6rYykrJ%2BZnq6ubrfAs6BnoKSiuQ%3D%3D